SIDO YAWATAKA WATANZANIA KUPENDA BIDHAA ZA NDANI

SIDO YAWATAKA WATANZANIA KUPENDA BIDHAA ZA NDANI

Like
404
0
Wednesday, 25 February 2015
Local News

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja

wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya amesema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja mmoja.

Amesema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi,

zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na dhana ya kununua bidhaa za nje wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la soko.

Comments are closed.