RAIS Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa msako wa nyumba kwa nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari wa ebola, na amepiga marufuku biashara kufanyika siku ya Jumapili.
Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, Rais Koroma ametoa amri ya kuzuia usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka shirika la afya Duniani WHO, Sierra Leone ni taifa ambalo limeathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa wa ebola ambapo zaidi ya matukio elfu nane yameripotiwa.