SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KUADHIMISHWA MWANZA KESHO

SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KUADHIMISHWA MWANZA KESHO

Like
394
0
Monday, 02 May 2016
Local News

TANZANIA leo inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza Mei tatu.

Katika maadhimisho ya Mwaka huu kubwa linalohimizwa na wadau wa Habari nchini ni kuitaka Serikali kuharakisha kupitisha Sheria ya Vymbo vya Habari kwa kuzingatia maoni yanayotokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali.

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaenda sambamba na matukio muhimu matatu ya kihistoria ya kuadhimisha miaka 250 ya Sheria ya kwanza ya uhuru wa Habari Duniani, ambapo kauli mbiu inasema “kupata Habari ni haki yako ya msingi, idai”.

Comments are closed.