MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amesema atawachukulia hatua kali, baadhi ya madiwani wateule wa wilaya hiyo ambao watasababisha vurugu na kuchochea migogoro kwa wananchi.
Kambona ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Loiborsoit A, kata ya Emboreet, ambapo amewataka madiwani hao watatue migogoro ya Ardhi bila kuathiri usalama uliopo kwa watu.
Aidha amewataka viongozi hao kutowashawishi wananchi na kusababisha vurugu badala yake watumie hekima na busara kutatua migogoro ya ardhi iliyopo.