SIMBA NA YANGA KUKICHAPA KESHO KWENYE MCHEZO WA LIGI KUU

SIMBA NA YANGA KUKICHAPA KESHO KWENYE MCHEZO WA LIGI KUU

Like
381
0
Friday, 17 October 2014
Slider

Kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba, kimerejea nnchini kimyakimya toka Afrika kusini baada ya kumaliza kambi yake na sasa wapo tayari kuwavaa watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa ligi kuu uatakaopigwa keshokutwa jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Daresalaam.

ikiwa huko Afrika kusini Simba chini ya kocha wake Mzambia Patrick Phiri, imecheza mechi tatu za kujipima nguvu, ambapo imekwenda sare mechi mbili na kuchezea kichapo mechi moja

Tumezungumza na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tulli, na kuthibitisha kuwasili kwa kikosi hicho, lakini pia ameeleza kuwa mlinda mlango wao namba 2 Husen Sharifu maarufu kama Casilas amejiondoa rasmi kushiriki katika mechi hiyo ya Octoba 18

Kwa upande wao Yanga kupitia mwenyekiti wake wa mashindano, Seif Ahmed maarufu kama Seif Magari, wamesema kikosi hicho chini ya kocha Mbrazil Maxio Maximo, kipo kamili na kinachosubiriwa ni muda tu ufike wa kumchinja mnyama

Comments are closed.