SIMBA YAKATAA KUKIPIGA NA YANGA LIGI KUU

SIMBA YAKATAA KUKIPIGA NA YANGA LIGI KUU

Like
354
0
Thursday, 24 November 2016
Slider

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kwa sasa hawatacheza mechi yeyote ile dhidi ya Yanga endapo TFF itaendelea kupanga waamuzi wa hapa nyumbani.

Mkuu wa mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema kuwa kama wao viongozi wameamua kufanya hivyo kwani waamuzi wa hapa nyumbani wamekuwa hawatendi haki kwa upande wao kwani mara nyingi hutoa maamuzi tofauti juu yao.

“Angalia mechi yetu dhidi ya Yanga,Martine Saanya anakataa goli halali la Ibrahimu Hajibu baadae anakubali goli la mkono lililofungwa na Amisi Tambwe,mwamuzi anatoa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa nahodha wetu Jonasi Mkude pasipo kosa lolote inashangaza sana”alisema Manara.

Amesema kuwa TFF kwa sasa inatakiwa kupanga waamuzi kutoka nje ya nchi katika mechi kubwa ya watani wa jadi ili kuondoa mzozo huo na wao watakuwa tayari kulipa gharama za waamuzi hao endapo TFF itashindwa kufanya hivyo.

Tumeitisha mkutano wetu wa wanachama kwa ajili ya mabadiliko ya katiba, halafu tunasikia kuna mtu huyu anajiita Mohammed Kiganja (Katibu wa BMT) eti anasema kitakachoafikiwa siku hiyo wao hawakitambui wakati waziri mwenyewe amekubali.

Tunashangaa huyu Kiganja ni nani hasa mpaka atuendeshe kiasi hiki, sisi tunasema, katika hili hakuna wa kutuzuia, tutafanya mabadiliko ya katiba kama wanachama wakikubali, hakuna wa kutuingia katika katiba yetu hata kama serikali ilihali hatuvunji katiba ya nchi.

“Hivi kwa soka la sasa ni nani asiyependa mabadiliko, huyu Kiganja yeye amekuwa akijitokeza kwenye migogoro tu, kwa nini katika maendeleo hayupo, tumefuata sheria zote za kuitisha mkutano na tutaufanya bila ya kizuizi chochote kile,” alimaliza Manara.

Comments are closed.