SIMBA YAMTAKA HANS POP KUTOZUNGUMZA CHOCHOTE KUHUSU CLUB HIYO

SIMBA YAMTAKA HANS POP KUTOZUNGUMZA CHOCHOTE KUHUSU CLUB HIYO

Like
472
0
Thursday, 30 October 2014
Slider

Siku moja tu baada ya kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba kumpiga stop mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zakaria Hans pop kutozungumza chochote kuhusu Simba kwa kuwa taarifa zake hazina Baraka ya uongozi, mwenyekiti huyo wa usajili ameibuka na kusema hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kumzuia isipokuwa rais wa Simba pekee.

hans ameyazungumza hayo baada ya E.sports kutaka kujua msimamo wake baada ya kauli ya iliyotolewa jana na katibu wa Simba stephen Ally.

Wakati hayo yakiendelea Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara wanalambalamba Azam fc wanapanda basi kesho kuelekea Mtwara kuwafata vijana waliokatika hali mbaya kwa sasa Ndanda fc, ambao watashuka nao dimbani Nangwanda sijaona.

Msemaji wa Azam Jaffer Idd Maganga amezungumza na E.sports na kuthibitisha pia wachezaji wao waliokuwa majeruhi wamerejea katika hali nzuri.

Comments are closed.