SIMBACHAWENE AKABIDHI NYARAKA ZA UFADHILI KWA WATANZANIA 22 KUSOMA MAFUTA, GESI CHINA

SIMBACHAWENE AKABIDHI NYARAKA ZA UFADHILI KWA WATANZANIA 22 KUSOMA MAFUTA, GESI CHINA

Like
262
0
Monday, 17 August 2015
Local News

WAZIRI wa Nishati na madini Mheshimiwa George Simbachawene, amewataka Wanafunzi 22 wanaokwenda nchi ya Jamhuri ya Watu wa China kusomea maswala ya Mafuta na Gesi, chini ya ufadhili wa nchi hiyo, kuzingatia masomo watakayopata huko ili waweze kuwa na chachu ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania katika sekta ya nishati.

 

Ufadhili huo ni ufadhili wa tatu nchini kufuatia kuanza kwa ufadhili huo mwaka 2013, ambapo awamu ya kwanza walipelekwa wanafunzi nane, mwaka 2014 wanafunzi 10 na mwaka huu wanafunzi 22 ambapo tangu kuanza kwa ufadhili huo kuna wanafunzi 4 wa ngazi ya Uzamivu (PHD) na wanafunzi 36 ngazi ya Uzamili (Masters).

x6 x41 x32 x12

Comments are closed.