CHAMA Cha Wataalam wa Habari za afya Afrika-AHILA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wameandaa mikakati ya kusambaza taarifa muhimu za afya kwa wananchi kwa kutumia mitandao ya habari ikiwemo simu za mikononi
Akizungumza na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mkutano wa kumi na nne wa wataalam wa habari za afya Afrika, Makamu wa Rais Dokta AHMED BILALI amesema kuwa taarifa za afya kutoka kwa wataalam mbalimbali wa afya nchini zitawafikia wananchi wote mijini na vijijini kwa urahisi zaidi kupitia simu zao za mikononi…..DOKTA BILAL
Naye Naibu Waziri Viwanda na Biashara JANETH MBENE akiongea kwa niaba ya Waziri wa Afya Dokta SEIF RASHID amefafanua kuwa kupitia simu hizo taarifa za afya zitafikishwa kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia kujikinga na kutambua dalili za magonjwa mbalimbali.
…..JANETH MBENE