SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa Radio za Jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, ZAINAB OMAR MOHAMMED wakati akizundua kituo cha Radio ya Jamii Jimbo la Mkanyageni, Mkoani Pemba.