soko la samaki kwa sasa limepanda kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hali inayochangia kuuzika kwa bei ya juu tofauti na miezi iliyopita.
Akizungumza na Efm makamu mwenyekiti umoja wa wauza samaki -UASADA katika soko la samaki feli Bwana CHARLES MUSSA amesema kuwa mbali na mabadiliko ya hali ya hewa kuchangia kupatikana kwa samaki hao lakini pia hali hiyo inasababishwa na uhaba wa vifaa vya kuvulia.
MUSSA amebainisha kuwa kutokana na kutopatikana kwa wingi samaki hapa nchini, wanalazimika kuagiza samaki kutoka nje ambao pia huuzwa kwa bei ya juu sababu ya kuwa na mlomlongo katika uingizaji wake.