SPIKA AHAIRISHA BUNGE KUFUATIA KUTOELEWANA BAADHI YA WABUNGE

SPIKA AHAIRISHA BUNGE KUFUATIA KUTOELEWANA BAADHI YA WABUNGE

Like
276
0
Thursday, 02 July 2015
Local News

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa ANNE MAKINDA amelazimika kuahirisha kikao cha bunge kabla ya wakati kufuatia Muongozo ulioombwa na mbunge wa Ubungo mheshimiwa JOHN MNYIKA juu ya kubadili mfumo wa uwasilishwaji na upitishwaji wa miswada ambayo bado haijawasilishwa hali iliyosababisha kutoelewana kwa wabunge wa chama tawala na wabunge wa vyama vya upinzani.

Hali hiyo imekuja baada ya wabunge wa vyama vya upinzani kuonesha hali ya kuonewa kwa madai kuwa hawapewi nafasi ya kutosha katika kujadili miswada hiyo pamoja na kutosikilizwa kwa maoni yao juu ya miswada hiyo.

Awali  akijibu swali la mheshimiwa Ritha Kabati mbunge wa viti maalum leo Bungeni mjini Dodoma, Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu –TAMISEMI– Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA amewataka wabunge pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali kushiriki kikamilifu katika suala la usimamizi wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi katika maeneo yao ili kuleta manufaa kwa Taifa.

Comments are closed.