SPIKA PAUL RYAN AMPINGA DONALD TRUMP

SPIKA PAUL RYAN AMPINGA DONALD TRUMP

Like
250
0
Friday, 06 May 2016
Global News

SPIKA wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani Paul Ryan amesema hayupo tayari kumuunga mkono Donald Trump kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.

Mfanyabiashara huyo bilionea anaonekana dhahiri kushinda katika mbio za uteuzi kukiwakilisha chama hicho lakini Ryan amesema kuwa kabla hakuweza kuidhinisha suala hilo Trump alipaswa kuwaonyesha watu kuwa anaheshimu taratibu za Republican na angepata kura za Wamarekani wengi zaidi.

Mapema Marais wa zamani wa Marekani George W Bush na baba yake George Bush waliweka wazi kuwa hawatunga mkono kupita kwa Trump.

Comments are closed.