STARS KUMENYANA NA MALAWI JUMAPILI

STARS KUMENYANA NA MALAWI JUMAPILI

Like
200
0
Wednesday, 25 March 2015
Slider

Timu ya taifa ya Malawi (The Flames) inatarajiwa kuingia nchini hapo kesho siku ya alhamisi ukiwa ni msafara wa watu 25 watakaotua uwanja wa taifa wa Mwl. Jk Nyerere ambapo siku ya ijumaa wanatarajiwa kutua katika jiji la Mwanza tayari kwa mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Stars siku ya jumapili.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).

Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe – Congo DR), Frank Banda (HBC Songo – Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol – Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United – Zimbambwe).

 

Comments are closed.