STARS YAFA KIUME UTURUKI

STARS YAFA KIUME UTURUKI

Like
234
0
Friday, 28 August 2015
Slider

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania taifa stars charles boniface mkwasa amesifia kuimarika kwa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo baada ya kuonesha makali katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya libya.

Mkwasa amesema kuwa kuna matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kuwania AFCON 2017 dhidi ya Nigeria baada ya washambuliaji hao kufanya vyema katika mchezo huo wa kirafiki pamoja na kupoteza kwa goli mbili kwa moja.

Aidha mkwasa amewatoa hofu watanzania kuelekea mchezo dhidi ya Nigeria tarehe 5 mwezi wa tisa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kwa kusema kuwa anafurahishwa na mwenendo mzuri wa timu hiyo katika kambi huko nchini Uturuki.

Comments are closed.