MATAIFA makuu duniani yamewapa muda viongozi wa pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini kuhakikisha wanakubaliana na kuhakikisha kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar anarejea Juba ifikapo kesho.
Mataifa hayo yamesema kuwa wakishindwa kukubaliana, makubalianao ya amani yaliyolengwa kumaliza miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yatavunjika.
Siku ya Jumamosi April 23 imewekwa na wawakilishi wa halmashauri ya JMEC iliyoundwa na Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, China, Uengereza, Norway na Marekani ambapo Sudan Kusini ni mwanachama wa halmashauri hiyo.