SUDAN KUSINI YAKABILIWA NA UKOSEFU WA CHAKULA

SUDAN KUSINI YAKABILIWA NA UKOSEFU WA CHAKULA

Like
199
0
Tuesday, 15 December 2015
Global News

MIAKA miwili tangu machafuko yalipoanza Sudan kusini, mashirika ya misaada yametahadharisha kuhusu upungufu mkubwa wa chakula unaotarajia kuikumba nchi hiyo na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kumaliza vitendo vya uhalifu wa kivita ndani ya Taifa hilo.

Ingawa makubaliano ya amani yalitiwa saini miezi kadhaa iliyopita, machafuko bado yanaendelea na karibu watu milioni moja na laki Tano wamelazimika kuyahama makazi yao.

Tangu kuanza kwa mapigano nchi nzima miaka miwili iliyopita, Rais na makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo wameshindwa kutekeleza makubaliano ya kuleta Amani.

 

Comments are closed.