SUDANI KUSINI: BASI LAVAMIWA

SUDANI KUSINI: BASI LAVAMIWA

Like
218
0
Thursday, 19 November 2015
Global News

BASI moja lililokuwa likisafiri kutoka mjini Juba kuelekea kampala nchini Uganda limevamiwa na kufyatuliwa risasi leo majira ya saa moja asubuhi.

Maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini wameeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Moli takribani kilomita 50 kutoka mji wa mpakani wa Nimule na kwamba kwa sasa bado wanaendelea kutafuta idadi kamili ya watu waliojeruhiwa.

Hata hivyo maafisa hao wamebainisha kwamba wanafanya jitihada za kukutana na kujadiliana na wenzao wa Uganda ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Comments are closed.