SUDANI KUSINI: SALVA KIIR AOMBA RADHI RAIA

SUDANI KUSINI: SALVA KIIR AOMBA RADHI RAIA

Like
256
0
Friday, 08 January 2016
Global News

RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mara ya kwanza amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kutokana na mateso na dhiki ambayo wamepitia wakati wa mzozo wa kisiasa uliodumu miaka miwili.

 

Rais  Kiir amesema kuomba msamaha ndiyo hatua ya kwanza katika kufanikisha maridhiano nchini humo.

 

Amechukua hatua hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano mkuu wa chama tawala cha SPLM. Jana, pande zilizohusika katika mzozo huo ziliafikiana kuhusu kugawana nyadhifa za uwaziri katika baraza la mawaziri la serikali ya umoja.

Comments are closed.