SUGE KNIGHT AKABILIWA NA KESI YA MAUAJI YA RAFIKI YAKE

SUGE KNIGHT AKABILIWA NA KESI YA MAUAJI YA RAFIKI YAKE

Like
373
0
Friday, 30 January 2015
Entertanment

Marion “Suge” Knight alihusika katika kugonga na kukimbia alasiri ya Januari 29) hali iliyopelekea mtu mmoja kufa na mwingine kujeruhiwa katika jimbo la California. ofisi ya mwanasheria James E. Blatt, wakili wa Knight alithibitishia vyombo vya habari

Kulingana na TMZ, Knight alikuwa katika mabishano na watu wawili juu ya seti ya filamu ambapo walinzi walimuamuru aondoke sasa wakati anaondoka kwa hasira aliwasha gari lake na kurudi nyuma kwa kasi na kumgonga rafiki yake yake aliekwenda nae eneo hilo Terry Carter

Chanzo kimeeleza kwamba Terry Carter alitaka kuingia kwenye gari hilo kupitia mlango wa nyuma na bahati mbaya akakanyagwa na gari hilo na kujeruhiwa vibaya hali iliyopelekea baadae kutangazwa kuwa amefariki na huku majeruhi mwingine hali yake ya kiafya haijajulikana hadi sasa.

Mpaka sasa mwanasheria wa Kinght hajathibitisha iwapo ni kweli Knight ndie aliekuwa akiendesha gari hilo

ABC news imeeleza kuwa Maafisa wa polisi wanachunguza kesi hiyo ambapo knight anatrajiwa kujisalimisha katika mamlaka husika

Pia imeripotiwa kuwa Ice Cube na Dr. Dre walihusika katika movie hiyo ila wakati ugomvi unatokea hawakuwepo katika eneo la tukio

 

Comments are closed.