SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA AMABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI

SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA AMABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI

Like
289
0
Tuesday, 29 March 2016
Local News

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es salaam na kufanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 yamefikishwa mahakamani  baada ya kukiuka masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.

 

Hayo yamebainishwa leo na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA David Mziray wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili abiria nyakati za asubuhi na Jioni.

 

Aidha Mziray amesema kati ya Machi 21 hadi 24 mwaka huu Sumatra imefanya ukaguzi huo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

Comments are closed.