SUMATRA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MAJINI KUKATIA LESENI VYOMBO VYAO

SUMATRA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MAJINI KUKATIA LESENI VYOMBO VYAO

Like
344
0
Thursday, 19 February 2015
Local News

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini-SUMATRA imewataka wamiliki wote wa Vyombo vya Majini kuhakikisha wanakatia Leseni vyombo vyao ili kuweza kufanya kazi kwa lengo la kupunguza vifo vya Majini. Rai hiyo imetolewa na Afisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoani Tanga WALUKANI LUHAMBA katika kikao cha maofisa na Mamlaka zinazojishughulisha na ukaguzi wa vyombo vya majini mkoani humo. Amesema vyombo vingi vya majini vimekuwa vikifanya kazi bila ya kufuata taratibu kitu ambacho ni hatari kwa maisha ya wasafiri wa vyombo hivyo.

Comments are closed.