WAZIRI Mkuu mstaafu mheshimiwa FREDERICK SUMAYE leo ametangaza rasmi nia ya kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi na kuhidi kuwa endapo atapewa ridhaa hiyo atahakikisha anawakwamua watanzania katika umaskini na kupambana na maovu.
Mheshimiwa SUMAYE ametoa ahadi hiyo jijini Dar es salaam wakati akiongea na wananchi juu ya malengo yake katika kulisaidia Taifa kukua kimaendeleo na kuingia katika ushindani wa kiuchumi.
Aidha akiwahutubia wananchi Waziri huyo mstaafu amebainisha kwamba anazo sifa zote za kuwaongoza wananchi katika kuleta usawa na kukomesha masuala ya rushwa.