SYRIA: BASHAR AL ASSAD AMEKIRI KUPUNGUA KWA MAJESHI YAKE

SYRIA: BASHAR AL ASSAD AMEKIRI KUPUNGUA KWA MAJESHI YAKE

Like
215
0
Monday, 27 July 2015
Global News

RAIS wa Syria Bashar al Assad amekiri kuwa idadi ya wanajeshi wake imepungua lakini amesisitiza kuwa bado jeshi hilo lina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji wa makundi ya waasi.

Assad ambaye aliuhutubia umma hapo jana katika mji mkuu wa Syria, Damascus pia amesema juhudi zozote za kuvikomesha vita nchini mwake ambazo hazitazingatia suala la kupambana dhidi ya ugaidi hazitakuwa na tija yoyote.

Jeshi la Syria ambalo wakati mmoja lilikadiriwa kuwa na wanajeshi laki tatu limepungua kwa asilimia 50 kutokana na kuuawa kwao, kuasi na wengine kukimbia vita hivyo.

Comments are closed.