MASHAMBULIZI makubwa ya mabomu yaliyofanywa na vikosi tiifu kwa rais Assad yameua jumla ya raia 18 katika mji wa Kaskazini mwa Syria wa Allepo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika la haki za binadamu linalofuatilia hali nchini humo,vikosi vya serikali vimefyatua makombora dhidi ya eneo la Al-Shaar mashariki mwa mji huo
Rami Abdel Rahman kiongozi wa shirika la haki za binadamu amesema makombora yamefyatuliwa dhidi ya mkusanyiko wa watu uliokuwa katika eneo hilo na kujeruhi watu kadhaa huku wengine wakiwa bado wamenasa chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.