SYRIA: MATAIFA YAAFIKIANA KUSITISHA MAPIGANO

SYRIA: MATAIFA YAAFIKIANA KUSITISHA MAPIGANO

Like
229
0
Friday, 12 February 2016
Global News

MATAIFA yenye ushawishi duniani yameafikiana kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano nchini Syria ambao utaanza kutekelezwa katika kipindi cha wiki moja ijayo.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo nchini Ujerumani.

Mwafaka huo hata hivyo hautahusisha makundi ya kijihadi ya Islamic State (IS) na al-Nusra Front. Aidha, Mawaziri wa mataifa wanachama wa Kundi la Kimataifa la Kusaidia Syria pia wamekubaliana kuharakisha na kuongeza juhudi za kutoa misaada.

Comments are closed.