MJUMBE wa Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura anatarajiwa kukutana na waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi kujadiliana kuhusu juhudi za kunusuru kuvunjika kwa mkataba wa amani nchin Syria.
De Mistura anataka Urusi na Marekani ambazo zinaunga mkono makundi pinzani nchini humo kushirikiana ili kurejesha makubaliano waliopatana mwezi Februari.
Hata hivyo Washington imeilaumu Moscow kwa kushindwa kuwazuia wanajeshi wa Syria waliopo mjini Aleppo.