SYRIA: UN YATOA MSAADA MADAYA

SYRIA: UN YATOA MSAADA MADAYA

Like
185
0
Monday, 11 January 2016
Global News

UMOJA wa mataifa umesema kuwa misafara ya magari iliyobeba chakula cha mwezi mzima na dawa leo umeanza kuelekea nchini Syria katika mji wa Madaya eneo ambalo limeathiriwa na njaa ambapo baadhi yao wamekufa kutoka na hali hiyo.

 

Watu zaidi ya elfu 40 wamezuiwa na serikali kutoka katika maeneo hayo na hawajahi kupokea msaada wa chakula tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

 

UN wanasema kuwa wanaushahidi kwamba baadhi wamekufa kwa njaa katika mji huo wa Madaya nchini Syria kutokana na msimamo wa serikali kutoruhusu mashirika ya misaada kuingi eneo hilo kutokana na mapigano.

Comments are closed.