RAIS wa Syria Bashar al-Assad amesema anatafakari mpango wa Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano katika mji wa kaskazini wa Aleppo.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura , amependekeza wazo hilo mwezi wa Oktoba wakati wa ziara yake katika eneo la vita.
de Mistura ameshauri kufanya majadiliano na kupata usitishaji wa mapigano ndani ya eneo hilo ili kuruhusu upelekaji wa misaada na kuweka mpango kwa ajili ya mazungumzo ya amani.