SYRIA YATAFAKARI KUSITISHA MAPIGANO ALEPPO

SYRIA YATAFAKARI KUSITISHA MAPIGANO ALEPPO

Like
229
0
Tuesday, 11 November 2014
Global News

RAIS wa  Syria Bashar al-Assad  amesema anatafakari  mpango  wa Umoja  wa  Mataifa kusitisha  mapigano  katika  mji  wa  kaskazini wa  Aleppo.

Mjumbe  wa  Umoja  wa  Mataifa  nchini  Syria  Staffan de Mistura , amependekeza  wazo  hilo mwezi  wa  Oktoba  wakati  wa  ziara yake  katika  eneo  la  vita.

de Mistura  ameshauri kufanya  majadiliano na  kupata usitishaji  wa mapigano ndani ya eneo hilo ili kuruhusu upelekaji wa misaada na kuweka mpango kwa ajili  ya  mazungumzo  ya  amani.

 

Comments are closed.