VIKOSI vya Jeshi nchini Syria na washirika wake vimedhibiti tena mji wa Al-Qaryatain kutoka mikononi mwa Islamic State, ukiwa ni muendelezo wa mapambano dhidi ya kundi hilo.
Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya kundi la IS kuondolewa katika eneo la karibu na mji wa Palmyra.
Wanamgambo wa IS waliuteka mji wa Al-Qaryatain mwezi Agosti, na kuwateka mamia ya wakazi wa mji huo wakiwemo Wakristo ambao wengi wao waliachiwa huru baadae.