TAASISI NCHINI ZIMETAKIWA KUKITUMIA KITUO CHA KISASA CHA KUHIFADHI TAARIFA

TAASISI NCHINI ZIMETAKIWA KUKITUMIA KITUO CHA KISASA CHA KUHIFADHI TAARIFA

Like
293
0
Wednesday, 09 March 2016
Local News

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote.

 

Akizungumza baada ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, sekta ya Mawasiliano Profesa Mbarawa amesema asilimia 75 ya kituo imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali.

 

Mbali na hayo amezitaka taasisi mbalimbali ikiwemo Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutembelea kituo hicho kujifunza mifumo ya uhifadhi taarifa na kujiunga ili kunufaika na huduma zinazotolewa.

Comments are closed.