TAASISI YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI CILT YATARAJIA KUFANYA MKUTANO MKUU WA KIMATAIFA

TAASISI YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI CILT YATARAJIA KUFANYA MKUTANO MKUU WA KIMATAIFA

Like
376
0
Thursday, 05 February 2015
Local News

TAASISI ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania- CILT inatarajia kufanya mkutano mkuu wa kimataifa utakaohusisha nchi mbalimbali za bara la Afrika kuanzia machi 4 mwaka huu.

Mkutano huo utahudhuriwa na wanachama wa CILT, Maafisa wa Sekretarieti ya Taasisi hiyo makao makuu mjini londan, wanachama kutoka nchi zingine nje ya Africa sambamba na viongozi wa Taasisi za uchukuzi wa lojistiki na wadau wengine.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Taasisi ya CILT barani Afrika BRIGEDIA GENERALI HARRISON MASEBO amesema kuwa Mkutano huo utakuwa ni mkutano wa 13 ambapo kwa Tanzania utafanyika kwa mara ya 4 ukiwa umelenga kujadili mada mbalimbali zitakazo wasilishwa na wataalam wabobezi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

 

Comments are closed.