TAASISI za Kifedha, Binafsi na Washirika wa Maendeleo nchini wameshauriwa kuzitumia nafasi zilizopo katika sekta ya nishati hususani umeme kwa kushirikiana na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini –REA– ili kujiletea maendeleo.
Hayo yamebainishwa na washirika wa Maendeleo katika tasnia ya nishati, kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujadili namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuhakikisha vijiji vinaunganishwa na nishati ya umeme.
Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava amesema miradi ya kuviunganisha vijiji na nishati ya umeme ni eneo linalohitaji kuendelezwa kwa ushirikiano na wadau hao ili kuongeza kasi yaZoezi hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya REA Edmund Mkwawa, akiongea jambo wakati wa kikao kazi baina ya REA, taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo na Taasisi Binafsi, Wizara , Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao hicho.