TACAIDS KUADHIMISHA SIKU YA UKIMWI NJOMBE

TACAIDS KUADHIMISHA SIKU YA UKIMWI NJOMBE

Like
326
0
Friday, 21 November 2014
Local News

 

TUME ya kudhibiti Ukimwi-TACAIDS inatarajia kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani ambapo mwaka huu maadhimisho hayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Njombe.

Maadhimisho hayo yatakayoanza Novemba 24 hadi Disemba Mosi mwaka huu, yamebeba kauli mbiu isemayo Tanzania bila maambukizo , ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sera, Mipango ya utafiti wa Tume hiyo Dokta Raphael Kalinga, amesema asilimia 99 ya watanzania wamesikia kuhusu Ukimwi na kati yao asilimia 60 tu ndiyo wanaelewa.

 

Comments are closed.