Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma stashahada (diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 kama ilivyokuwa imetangaza Mei 10 mwaka huu. HESLB ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 ambao ulieleza kuwa ingeanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ungetolewa baadaye. Hata hivyo, taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru inasema hatua hiyo...