Rais Magufuli amemteua Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Aidha, amemteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Rais Magufuli amemteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Rais Magufuli amemteua Ndg. Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na Ndg. Lengay Ole Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Pia amemteua Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akichukua nafasi ya Ally...
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi. Makamo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya ukombozi Afrika, Mwebesa Rwebugia ameieleza BBC kwamba rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasaa katika ukuaji wa miundo mbinu. Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika. Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa,...
RAIS Dkt. John Magufuli ametangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa eneo la Mbezi Jijini Dar es Salaam kuendelea kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara huku akizitaka mamlaka husika zisiwanyanyase wafanyabiashara hao wanaotafuta kipato . Dkt. Magufuli ameeleza hayo jana Julai 16, 2018 wakati akiwa njiani kuelekea Ikulu akiwa anatokea Mkoa wa Pwani, Kibaha kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere na kusema wafanyabiashara hawawezi kunyanyaswa katika kipindi chake ambacho atakuwa madarakani huku akiwataka...
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais leo July 13, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Uteuzi huu umeanza leo July 13, 2018. Kabla ya uteuzi huu Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga, DSM. Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike anachukua nafasi ya Dkt. Juma Alli Malewa ambaye amestaafu....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatambulisha Baadhi ya Viongozi (hawaonekani pichani ) kwa Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiiongozi Balozi John Kijazi akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam ili kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu na viongozi wastaafu ambao anakutana nao kwa mara ya kwanza wote kwa pamoja. Viongozi Wakuu wastaafu wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam tayari kukutana na...
Dkt. Bashiru Ally amepitishwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana. Dkt. Bashiru amepitishwa leo Mei 29, 2018 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama(NEC) Dkt. Bashiru ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume maalum ya kuchunguza mali za CCM iliyoundwa na Rais Magufuli PICHA NA...
Rais Magufuli Atoa Wito kwa Majeshi Yote Nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Mei, 2018 amezindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo katika kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani (831KJ) Jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kina viwanda vya kushona nguo, kutengeneza maji, kukereza vyuma na pia kina chuo cha ufundi stadi (VETA), shule ya sekondari Jitegemee na kumbi mbili za...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo Alhamisi Mei 17, 2018 amefungua kituo cha Uwekezaji cha Suma JKT kilichopo Mgulani. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo mawaziri, pamoja na maafisa mbalimbali wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini. Katika hafla hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ameeleza kuwa JWTZ linazidai sekta binafsi kiasi cha shilingi bilioni 40, huku taasisi...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya...