mambo sasa

Askari wawili wahojiwa tukio la mwanahabari kupigwa
Global News

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema polisi waliokuwa zamu siku ambayo mwandishi wa habari wa Wapo Redio, Sillas Mbise alishambuliwa na askari, wameanza kuchunguzwa. Mbise anadaiwa kushambuliwa na polisi juzi Agosti 8, 2018 wakati wa mchezo kati ya Simba na Asante Kotoko ya Ghana uliofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Amesema jukumu la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao na si kuwapiga raia waliotenda kosa ambao hawajakataa kutii sheria...

Like
560
0
Friday, 10 August 2018