Miaka tisa tokea dunia ipate taarifa za kifo cha mfalme wa muziki wa Pop duniani Marehemu Michael Jackson ambaye alifahamika duniani kote kutokana na upekee aliokuwa nao katika uchezaji pamoja na nyimbo zake ambazo zilipendwa na watu wengi ulimwenguni. Marehemu Michael Jackson alipendwa zaidi na watoto kutokana na upendo na ukaribu aliokuwa nao kwa watoto wote ambapo hakujali rangi na enzi za uhai wake Michael Jackson aliwahi pia kutembelea Tanzania na kukutana na Rais wa awamu ya pili wa Tanzania...