Rais wa Marekani Donald Trump anakusudia kumwalika Washington, Rais wa Urusi Vladmir Putin baadaye mwaka huu, licha ya kuendelea kuwepo ukosoaji juu ya mkutano wao uliofanyika Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Finland Helsinki. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sara Sanders amesema majadiliano kuhusiana na ziara hiyo tayari yameanza. Hata hivyo, Kiongozi wa maseneta kupitia chama cha Democrat nchini humo Chuck Schumer ameupinga mualiko huo mara moja kwa kusema kuwa Rais Trump hapaswi tena kukutana ana kwa ana na...
Vyombo vya habari vya taifa nchini Uturuki vimetangaza kwamba serikali imeondoa hali ya hatari iliyowekwa nchini humo kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa miaka miwili iliyopita. Katika kipindi hicho makumi kwa maelfu ya watu walikamatwa na kushikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka chini ya agizo la Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan. Wanajeshi, Polisi, Raia, Waandishi wa Habarai na walimu ni miongoni mwa waliokamatwa. Maelfu wengine ikiwemo majaji kadhaa waliachishwa kazi zao. Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema...