Kiungo mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil amesema hataki tena kuiwakilisha Ujerumani katika michuano ya kimataifa. Katika taarifa ndefu iliyotolewa na Ozil mwenye miaka 29, imesema kufanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana na chama cha soka cha Ujerumani DFB, kumemfanya asitake tena kuivaa jezi yao. Ameongeza kuwa amekuwa akilaumiwa sana kwa Ujerumani kufanya vibaya katika michuano ya kombe la dunia. Mwezi May, Ozil alilalamikiwa vikali na mashabiki pamoja na chama cha soka cha Ujerumani kwa kupiga picha na Rais wa Uturuki Recep...
Mesut Özil (kushoto) alimkabidhi rais Erdogan jezi yake ya Arsenal Nyota watatu wa Uturuki walipiga picha na bwana Erdogan (kutoka kushoto): Ilkay Gündogan (Man City); Mesut Özil (Arsenal) na Cenk Tosun (Everton) Shirikisho la soka Ujerumani (DFB) limeshutumu wachezaji wake wa kimataifa Mesut Özil na Ilkay Gündogan kwa kupiga picha na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Wachezaji hao wawili waliozaliwa Ujerumabni, wote wenye asili ya Kituruki, walimkabidhi Erdogan fulana zao walizozisaini katika hafla moja mjini London siku ya Jumapili....