WAZIRI wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk. Saleh Ali Sheikh amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine kutokana na amani iliyopo. Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumapili, Mei 27, 2018) wakati akitoa nasaha kwa wageni walioshiriki futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi yake jijini Dar es Salaam. “Ninaomba nipelekewe shukrani zangu kwa umma wa Watanzania kutokana na upendo walionao. Ukiwaona ni watu wa amani, furaha na upendo na hili linathibitishwa na...