Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani wamejibizana vikali na kutoa vitisho huku uhasama baina ya mataifa hayo mawili ukizidi. Bw Trump ameandika kwenye Twitter, kwa herufi kubwa, kwamba “Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia” iwapo itaitishia Marekani. Bw Rouhani awali alikuwa amesema kwmaba vita na Iran vitakuwa “vita zaidi ya vita vingine vyote”. Mwezi Mei, Marekani ilijitoa kutoka kwa mkataba wa nyuklia na Iran ambao ulikuwa umehusisha Iran...
Rais wa Marekani Donald Trump na wa Urusi Vladmir Putin muda mchache ujao watakutana kwa mazungumzo, katika makazi ya Rais wa nchi hiyo mjini Helsinki, ambao ni mkutano wao wa kwanza kabisa kuwakutanisha pamoja. Mpaka sasa hakuna ajenda yoyote ya mkutano huo, ambao utahudhuriwa tu na watafsiri wao. Aidha licha ya mkutano huo kutotegemewa sana, lakini wanaweza kuonesha dalili mpya za kuanza kwa awamu mpya ya mahusiano kati ya Washngton na Moscow, baada ya kufarakana kufuatia Urusi kuitwaa kwa nguvu...
Katika hatua nyingine Trump ameilaumu Ujerumani kwa madai kwamba inatumia kiasi kidogo, katika bajeti ya ulinzi wakati ambapo inatumia fedha nyingi katika ununuzi wa bidhaa za nishati, kutoka nchini Urusi,taifa ambalo walipa kodi wa Marekani wanachangia kodi zao kukabiliana na vitisho vyake. Kansela wa Ujeruman Bi Angela Merkel,amejibu shutuma hizo za Trump na kudai idadikubwa ya wanajeshi wake wapo katika vikosi vya NATO Bi Merkel Anasema “sisi ni taifa la pili kuwa na kikosi kikubwa cha wanajeshi wetu,tunanatoa mchango mkubwa...
Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili Singapore kwa ajili ya mkutano wao unaoelezwa kuwa wa kihistoria. Trump aliwasili saa chache tu baada ya Kim kuwasili na ujumbe wake. Mkutano wao ambao ni wa kwanza utafanyika siku ya Jumanne katika kisiwa cha Sentosa. Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili...
Rais Trump ametilia shaka kufanyika mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi june huko Singapore . Amesisitiza kuwa hata hivyo Korea kaskazini itapaswa kutimiza vigezo vilivyowekwa ambayo ni nadra kutokea. Korea Kaskazini ilikwisha sema kuwa inaweza kujiondoa katika mkutano huo iwapo Marekani inasisitiza suala la kuachana na mpango wa silaha za nyuklia. Rais Trump amezungumzia mkutano huo,mara baada ya kumpokea katika ikulu ya Marekani rais wa Korea Kusini Moon Jae-in. Hata hivyo rais trump hakuweka wazi ni...
Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia. Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni. Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea. Maandalizi ya mkutano huo wa Trump-Kim yamekuwa yakiendeleza,...
Marekani itafungua ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa. Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner. Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria. Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umewakasilisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye. Ambao waliudhibiti toka...
Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi ” kutumia nguvu ” kujibu madai ya shambulio la kemikali nchini Syria, huku mataifa ya magharibi yakitafakari hatua watakayoichukua. “Tuna njia nyingi za kijeshi,”aliwambia waandishi wa habari. Aliongeza kuwa hatua ya kujibu shambulio hilo itaamuliwa katika kipindi cha “muda mfupi”. Bwana Trump alisema kuwa Marekani inapata ”msaada mzuri” juu ya nani aliyehusika na shambulio la Douma Jumamosi. Duru za kitabibu zinasema makumi kadhaa ya watu waliawa...