Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 20, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo. Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto,wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo,huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens. Kikosi cha uokoaji kinaendelea na jitihada za kuwapata watalii 10 ambao walitoweka katika harakati za kujiokoa na moto huo. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis...