Amnesty International imelaani mamlaka nchini Iran kwa kumchapa viboko hadharania mwanamume ambaye alipatikana na hatia ya kunywa pombe wakati alikuwa na umri wa miaka 14. Vyombo vya habari vilichapisha picha za mwanamume ambaye alitambuliwa kama “M R” akichapwa viboko 80 kwenye mji ulio mashariki wa Kashmir siku ya Jumanne. Waendesha mashtaka wanasema alikamatwa wakati wa maadhimisho ya mwaka wa Iran wa 1385 wa kati ya (Machi 2006 na Machi 2007) na alihukumiwa mwaka uliopita. Haijulikani sababu iliyochangia adhabu hiyo kuchukua...