Marekani Jumatano imeweka vikwazo kwa watendaji 15 wa mafuta wa Sudan Kusini ambao imesema walikuwa vyanzo muhimu cha fedha kwa serikali, hatua ambayo inalenga kuongeza shinikizo kwa rais Salva Kiir kumaliza mgogoro na mzozo wa kibinadamu nchini kwake. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters makampuni na taasisi za serikali huenda katika siku za mbeleni zikahitaji leseni maalum ya kufanya biashara nchini Marekani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema. Serikali ya Sudan Kusini na maafisa ambao ni...