WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hakuna michango yoyote itakayokusanywa kutoka kwa wazazi kwa ajili ya shule kama haina kibali cha Mkurugenzi wa Halmashuri. “Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli alishapiga marufuku michango ya aina hii na akatangaza mpango wa elimumsingi bila malipo. Sasa hivi zinaletwa zaidi ya sh. bilioni 20 kila mwezi kwa ajii ya kuboresha elimu ya msingi katika kila wilaya.” Waziri Mkuu ametoa katazo hilo jana (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria...
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini wasibaki nyuma katika suala zima la kuwekeza kwenye viwanda ili waweze kuendana na azma ya Serikali ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. “Serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi wa viwanda. Nawaomba msiwe nyuma katika suala hili, tumieni fursa ya ardhi tuliyonayo hasa katika ujenzi wa viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao,” amesema. Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo Alhamisi, Julai 12, 2018 wakati akifungua...
...