Baada ya siku takribani tano kupita tangu kikosi cha Yanga kiweke kambi mjini Morogoro, imeelezwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ameomba mechi moja kukipima kikosi chake. Taarifa kutoka Morogoro zinasema Zahera ameomba apatiwe timu moja ambayo haishiriki Ligi Kuu Bara ili aweze kukipima vizuri kikosi chake kabla ya kufikia hatua ya kucheza na timu za daraja la juu. Taarifa zinaeleza Yanga wametuma maombi kwa timu zaidi ya moja mjini humo na ambayo itakubali watakipiga nayo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi...
Baada ya viongozi wa Yanga kuzidi kuachia ngazi akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo jana, Clement Sanga kutangaza kujiuzulu wadhifa wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameitisha kikao na wahabari leo. Nyika ameitisha kikao hicho kuzungumzia mustakabali mzima wa Yanga juu ya kujaza nafasi za viongozi wake walioachia ngazi namna utakavyokuwa. Ikumbukwe Yanga imekuwa haina Mwenyekiti kwa muda mrefu tangu kujiuzulu kwa Yusuf Manji akidai anahitaji kupumzika kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi binafsi. Baada ya Manji,...
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amejiuzulu nafasi yake katika klabu hiyo kuanzia leo hii. Amesisitiza kuendelea kuwa mwanachama na kuisaidia klabu ya Yanga katika kila hali. Kwa upande wa hela zinazozungumziwa za Milioni 240 za kutoka CAF, Sanga amesema Yanga imekuwa na changamoto nyingi sana katika upande wa fedha na wamekuwa wana madeni makubwa ambayo wanakatwa katika mapato ya mlangoni ikiwemo Deni la Ardhi na madeni mengine...