TAIFA LITAPIGA HATUA IWAPO KILA MTU ATAWAJIBIKA KWA NAFASI YAKE KATIKA KAZI

TAIFA LITAPIGA HATUA IWAPO KILA MTU ATAWAJIBIKA KWA NAFASI YAKE KATIKA KAZI

Like
219
0
Monday, 20 April 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa iwapo kila mtu kwenye nafasi yake ya kazi atakaa nakujua anapaswa kufanya nini, akafanya kazi yake vizuri kama inavyostahili Taifa linaweza likapunguza kama sio kumaliza kabisa changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo na kuwezesha Taifa kupiga hatua kubwa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Anna kilango Malechela alipotembelea Mamlaka ya Elimu ya Tanzania-TEA.

Akizungumza na waandishi wa habari Mheshimiwa Malechela amesema hakuna sababu ya kuita Tanzania kuwa ni changa kwa kuwa ni watu wenyewe ndio wanaifanya ionekane changa na endapo watu watajitahidi kwa bidii nchi itasogea na kufika sehemu inayopaswa kuwa ki maendeleo.

Comments are closed.