MKURUGENZI wa Taasisi ya Takwimu nchini dokta Albina Chuwa amesema kuwa suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili bado ni ngeni katika nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika.
Dokta Chuwa ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya takwimu za hali ya mazingira kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki jijini Arusha uliohudhuriwa na viongozi wa Takwimu wa nchi hizo.
Amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia hali ya tabia nchi na mazingira huku akisisitiza kuwa Takwimu za mazingira zinahitaji watu wawe na uwezo mkubwa wa elimu pamoja na rasilimali fedha na vifaa huku akitoa rai kwa Jumuiya ya Afrika mashariki kuangalia tasnia hiyo kwa kuipa kipaumbele sawa na sekta zingine.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja
Washiriki wakifwatilia mafunzo kwa ukaribu zaidi